Tume yaahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata

Written By Admin on Sunday, October 31, 2010 | 10:54 PM

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KUAHIRISHA BAADHI YA CHAGUZI MBALIMBALI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa katika kikao chake cha tarehe 30/10/2010 imefanya maamuzi ya kuahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.

Kata na Majimbo ambayo Chaguzi zake zimeahirishwa ni kama ifuatavyo:-

1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa anzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)

2. Uchaguzi wa Madiwani katika kata zifuatazo:-


Na.
HALMASHAURI
KATA

1
Newala DC
Mtonya

2
Mbulu DC
Endegikot

3
Manyoni DC
Kitaraka

4
Same DC
Kisiwani

5
Kibaha DC
Janga

6
Rufiji
(a) Kibiti

(b) Chemchem

(c) Ngorongo

(d) Kipugira

(e) Mjawa

7
Uyui DC
(a)KIgwa

(b)Ibelamilundi

8
Sikonge
Kisanga

9
Njombe
Mji Mwema



10
Ulanga DC
Msogezi

11
Karagwe DC
(a) Kimuli

(b) Kamuli

12
Kasulu
Kitagata

13
Chato DC
Buseresere

14
Mwanza (Jiji)
(a) Mkuyuni

(b) Mirongo

Hata hivyo katika majimbo hayo matatu ambapo Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Madiwani utanaendelea kufanyika leo kama ilivyopangwa.

Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa.

Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa tarehe za kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa hapo baadaye.


(Rajabu R. Kiravu)

Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi

0 comments:

Post a Comment