Tovuti bora hujitenga na mbaya hujikusanya

Written By Admin on Sunday, August 21, 2011 | 9:53 PM


 

Tovuti bora hujitenga na mbaya hujikusanya

Usiwe kama wao,bali kuwa kama wewe
Katika dunia ya sasatumekuwa tukishuhudia mrundikano wa tovuti au programu ambazo kazi zake nyingi huwa zinafanana.Wetu wengi tumekuwa tukijitetea kuwa dunia ya leo hakuna cha kugundua kwani kila kitu kimeshagunduliwa,pia kuna wengine wanasema huwezi kuja na kipya kwakuwa tayari kuna vipya vingi.
Leo hii nitakupa mazingatio machache ambayo wewe kama mmiliki wa tovuti unatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha unakuwa na tovuti iliyo matata na manufaa.

1.Kuwa kama wewe

Epuka kukopi kila kitu ulichokiona kwenye tovuti fulani,kwa mfano leo hii kama utataka kutafuta makala za kitanzania kwenye mtandao,utajikuta kuna mrundikano wa makala nyingi ambazo ni sawa ila zinatoka kwenye vyanzo(tovuti) tofauti,hii ni kwa sababu kutokana na mtindo wetu wa kukopi kila kitu tunachokiona,siku ya mwisho watumiaji huanza kusema si wale wenye tovuti za…,kwenye …ninamaanisha mwanzilishi au mbabe kwenye hiyo idara,inakuwa ngumu kujitofautisha au kuteka akili za watembeleaji ikiwa hauna kitu cha kipekee.

2.Tengeneza mtandao

Kuna watu wanaweza kuanza kujiuliza ninamaanisha nini kusema mtandao ndani ya mtandao? Hapa ninamaanisha ushirikiano.Mara nyingi tovuti nyingi zimekuwa zikifa au kuishia njiani kutokana na kushindwa kuendeleza,hii inatokana na kukosa ushirikiano,ni ngumu mno kuendeleza tovuti peke yako.Siku hizi kuna njia nyingi mno ambazo unaweza kuzitumia kukuongezea mtandao au ushirikiano.Hakikisha unachunga kila kinachoingia na kutoka katika kuhakikisha unakuwa na tovuti ya kipekee.
Hayo ni madokezo machache ambayo kama utazingatia yatakusaidia kuwa na tovuti yenye manufaa na inayokubalika,

MAKALA HII KWA HISANI YA AFRO IT BLOG

0 comments:

Post a Comment