Waagizaji Wa Mafuta Wakubali Kuuza Mafuta Kwa Bei Mpya

Written By Admin on Thursday, August 4, 2011 | 10:23 PM

Waagizaji wa mafuta kutoka makampuni mbali mbali yanaoagiza na kuuza mafuta hapa nchini, wakiwa katika mkutano wao leo mchana Wizara ya Nishati na Madini,  Mkutano huo ulikuwa ukijadili kuhusu mgomo wa makampuni ya kuuza mafuta wanayoyamiliki uliotokana na serikali kupitia EWURA, kushusha bei za mafuta.Katika mkutano huo ulioongozwa na Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na viongozi wa EWURA, waagizaji na wauzaji hao  wa mafuta wamekubali kusitisha mgomo wao na kuendelea kuuza mafuta kwa bei mpya iliyotangazwa na EWURA.


source mjengwa blog

0 comments:

Post a Comment