NILIIPENDA SPURS ZAIDI YA LIVERPOOL.

Written By Admin on Tuesday, September 7, 2010 | 2:16 PM

Kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Rafael van der Vaart amesema almanusura angejiunga na klabu ya Liverpool kabla ya klabu yake ya zamani ya Real Madrid haijamuuza kwenye klabu ya Tottenham mnamo August 31 mwaka huu.


Rafael van der Vaart amesema dili la kujiunga na klabu ya Liverpool lilivunjika baada ya viongozi wa klabu ya Tottenham kukamilisha usajili wake dakika za mwishoni.


Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 17 amebainisha wazi kwamba viongozi wa klabu ya Liverpool walikua wanamfuatilia kwa ukaribu kabla hajaondoka huko St Bernabeu lakini walichelewa kukamilisha taratibu za uhamisho wake hivyo akaona ni bora ajiunga na Spurs ambao walikua tayari kumsajili.

Amesema licha ya kuisubiri kwa hamu klabu ya Liverpool imsajili, tayari mapenzi yake yalikua yameshaelekea kwenye klabu ya Spurs na angekua katika wakati mgumu endapo vilabu hivyo vingekuwa sambamba katika harakati za kumsajili nyakati za mwisho za usajili katika bara la Ulaya.


Mbali na vilabu hivyo viwili Rafael van der Vaart amedai klabu ya Bayern Munich nayo ilikua na malengo la kumsajili lakini akasisitiza kwamba yeye binafsi hakupendezewa na ofa hiyo na angejisikia vibaya endapo angesajiliwa na klabu hiyo inayotetea ubingwa wa ujerumani.

0 comments:

Post a Comment