Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajab Kiravu, jana jioni ilisema imepokea taarifa ya kuwapo mitihani hiyo. “Kwa kuzingatia kwamba mitihani hufanyika katika mazingira ya utulivu na amani na kwa kuwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mara kwa mara hufanyika karibu na maeneo ya shule za msingi, NEC baada ya kushauriana na vyama vya siasa imeamua kwamba pasiwepo kampeni kati ya Septemba 6 na 7.
Alisema kutokana na hali hiyo, tume hiyo imetoa maelekezo kwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu kuhakikisha wanasitisha mara moja kampeni katika majimbo yote kwa siku hizo. Pia NEC imewataka viongozi wa vyama vya siasa, wagombea na mawakala wao wahakikishe hawafanyi kampeni katika siku hizo zilizotajwa.
Hadi jana NEC inatoa tangazo hilo, tayari wagombea wa vyama mbalimbali wamesambaa mikoani kwa ajili ya kunadi sera zao. Mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekwisha kuzunguka zaidi ya mikoa sita ikiwamo Kigoma, Mwanza, Kagera, Dar es Salaam na Mbeya. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, yuko kwenye mikoa ya kusini akiendelea kunadi sera zake. Hali ikiwa hivyo, mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameendelea kuchanja mbunge katika mikoa mbalimbali ikiwamo Morogoro na Manyara. Mbali ya wagombea urais, pia kampeni za wagombea ubunge na udiwani nazo zimeendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali.
NEC yasitisha kampeni kupisha mitiana ya darasa la saba
Written By Admin on Sunday, September 5, 2010 | 4:52 PM
Labels:
NEWS,
POLITICS,
UCHAGUZI 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment