Muwekezaji mpya wa klabu ya Liverpool John Henry amewaaahidi mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo atafanya mapinduzi ya soka huko Anfiled ambapo kwa sasa kunafukuta kufuatia matokeo mabaya yanayowaandama.
Muwekezaji huyo ambae jana alipitishwa na kikao cha bodi ya viongozi wa klabu ya Liverpool amesema anaifahamu vilivyo klabu hiyo na alikua naifuatilia kwa ukaribu huku akibainisha wazi kwamba matatizo yaliopo sasa klabuni hapo ndio chanzo cha yeye kuamua kuingia kwenye harakati za kutaka kuiongoza The Reds.
Amesema soka ni mchezo ambao unahitaji maandalizi na yeye kwake suala hilo sio tatizo kwani ana mipango mizuri na madhubuti ambayo anaamini itakapoanza kufanyiwa kazi kila mmoja anayoipenda Liverpool atafurahishwa nayo.
John Henry ambae pia mmiliki klabu ya Boston Red Sox ya mchezo wa Baseball ya huko nchini Marekani ametoa angalizo kwa yoyote anaeipenda klabu hiyo kuhakikisha anatoa mchango wake wa kimawazo hatua ambayo anaamini itamsaidia kufikia malengo aliyojiwekea.
Tayari mwenyekiti wa muda wa klabu y Liverpool Martin Broughton amewataka wanaliverpool kuwa watulivu na kutambua kwamba kuuzwa kwa klabu yao kwa thamani ya paund million 300 ni sehemu ya kusaka mafanikio kama ilivyo kwenye vilabu vingine vilivyo chini ya wawekezaji nchini Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment