Yanga ndiyo timu pekee ambayo hadi sasa haijafungwa kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Baramsimu huu.
Mpaka mechi za raundi ya sita, Yanga imebaki kuwa timu pekee ambayo haijaonja machungu ya kipigo, baada ya Mtibwa Sugar iliyokuwa na rekodi hiyo sawa na Yanga kuchapwa bao 1-0 na Simba mkoani Morogoro juzi.
Yanga ilianza ligi kwa kuichapa Polisi ya Dodoma kwa goli 1-0, ikaiangushia kichapo 2-0 AFC ya Arusha, ikatoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, ikaichapa Majimaji ya Songea 1-0 , ikailaza Kagera Sugar mabao 2-0, kabla ya kuiangusha Ruvu Shooting kwa idadi hiyo hiyo ya magoli.
Hata hivyo, itakuwa na kibarua kigumu cha kuilinda rekodi hiyo Oktoba 16 wakati itakapocheza na mahasimu wao Simba ambao, tayari wametia doa rekodi ya Mtibwa.
Kabla ya kutibuliwa rekodi yao, Mtibwa ilianza ligi kwa kucheza na Majimaji na kushinda 1-0, ikatoka sare ya bila kufungana na Polisi Dodoma, pia ikatoka sare ya 1-1 na Yanga, ikaibwaga Kagera Sugar 2-1, ikatoka sare ya bila ya kufungana na JKT Ruvu, kabla ya kukumbana na kipigo toka kwa Simba.
CHANZO: NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment