NICOLAS ANELKA huenda akaihama CHELSEA

Written By Admin on Friday, August 19, 2011 | 10:01 AM

Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Chelsea Nicolas Anelka huenda akaihama klabu hiyo kabla ya august 31 ambapo itakuwa mwisho wa dirisha la usajili katika kipindi hiki.

Nicolas Anelka ambae alijumuishwa kikosini mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu, anafikiria kufanya hivyo kufuatia uhalisia wa upatikanaji wa nafasi ndani ya kikosi cha chelsea.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anakabiliwa na changamoto mbali mbali klabuni hapo kutokana na hatua ya kusajiliwa kwa Fernando Torres mwanzoni mwa mwaka huu, kurejea kwa mshambuliaji kinda Daniel Sturridge aliekua ametolewa kwa mkopo huko Bolaton wanderers pamoja na uwepo wa mshambuliaji mwingine Didier Drogba.

Taarifa zilizopo zinadai kwamba Nicolas Anelka anapewa nafasi ya kipekee ya kujiunga na Spurs ambao wapo tayari kuwaachia baadhi ya washambuliaji wao kama Jermain Defoe pamoja na Peter Crouch huku Robbie Keane akiwa tayari ameshajiunga na LA Galax

0 comments:

Post a Comment