Ndege ya kijeshi ya Uingereza imepeleka pauni milioni 950 Libya baada
ya Umoja wa Mataifa kuondoa tanji iliyokuwa imelengwa kwa Kanali
Gaddafi.
Noti, zilizotimia dinari za Libya bilioni 1.8 zilizochapishwa Uingereza, zitawasilishwa kwenye benki kuu ya Libya.
Afisa mmoja amesema fedha hizo zinatakiwa ziwepo
ili ziingizwe kwenye mashine ya kutolea pesa yaani ATM na kusambazwa
kwenye benki haraka iwezekanavyo.
Afisa huyo alisema fedha hizo zitasaidia kulipa wafanyakazi wengi wa sekta ya umma wakati wa likizo ya Eid.
Wengi ambao wanategemea mishahara ya serikali hawajalipwa katika kipindi cha wiki kadhaa.
Hatua hiyo inachukuliwa siku moja kabla ya
mkutano mkuu wa kimataifa juu ya hatima ya Libya unaotarajiwa kufanyika
mjini Paris siku ya Alhamis.
Mkutano huo utaongozwa kwa pamoja na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
0 comments:
Post a Comment