Mshauri wa baraza la kata Gongo la Mboto, anayekabiliwa na kesi ya kutishia kuua na kusababisha fujo, Ally Sururu (60) ametupwa lupango miezi sita, baada ya kukaidi amri ya pilato aliyemtaka avue kofia aliyokuwa ameivaa kizimbani aina ya baraghashia.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, WilbaForce Luhwago, mara baada ya mtuhumiwa huyo kumwambia hakimu huyo kuwa hana maadili kwa kumtaka yeye avue kofia.
Mara baada ya Sururu kutoa kauli hiyo mbele ya mahakama, hakimu Luhwago alimtaka akampumzike kwa muda katika mahabusu ya mahakama hiyo ya Ilala.
Lakini cha kushangaza, mtuhumiwa alikaidi amri hiyo huku akimweleza hakimu Luhwago kuwa baraghashia ni sawa na vazi lolote hivyo hawezi kuivua.
Hakimu Luhwago alimwambia mshtakiwa huyo kuwa kwa sababu hiyo ni tabia yako ya kudharau mahakama ukiachiwa utaendelea na tabia hiyo, hivyo utatumikia kifungo cha miezi sita jela huku kesi yako inaendelea kusikilizwa.
Sururu ambaye yupo nje kwa dhamana , kabla ya kuhukumiwa kifungo hicho cha miezi sita jela, jana hiyo alifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuisikiliza kesi yake.
Kabla ya kupewa hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Daniel Buma aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mtuhumiwa kutokana na tabia aliyoionyesha ya kudharau mahakama na kudaia kuwa zikiachiwa tabia hizo mahakama hazitaheshimiwa”alidai Buma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment