WAKATI kampeni za kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi wa kisiasa nchini zikizidi kushika kasi na kutawaliwa na vijembe na mbwembwe, imebainika kuwa mambo si shwari katika ngome ya Chama cha Mapinduzi (CCM).Mambo si shwari katika ngome hiyo kutokana na viongozi waandamizi wa kitaifa wastaafu wakiwamo marais wastaafu William Mkapa na Ali Hassan Mwinyi kususa kuwapigia debe wagombea wa chama hicho, akiwamo mgombea Urais, Jakaya Kikwete.
Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanasema badala ya viongozi hao kumsaidia Kikwete, familia yake ikiongozwa na mkewe Mama Salma ambaye yuko Kaskazini mwa nchi na mtoto wake, Ridhiwani, aliyeko Kusini ndiyo inayoendelea kuwashawishi Watanzania ili Kikwete aendelee kuwepo madarakani.
Viongozi wengine waandamizi ambao hawaonekani kwenye majukwaa ya kumnadi Dk. Kikwete ni pamoja na Mawaziri Wakuu wastaafu Frederick Sumaye, John Malecela, Cleopa Msuya na hata Jaji Joseph Warioba.
Rais Kikwete atoswa!!
Written By Admin on Friday, September 17, 2010 | 4:37 PM
Labels:
POLITICS,
UCHAGUZI 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment