Baada ya kuachwa kwenye kikosi cha Man Utd kilichocheza hii leo mchezo wa pili wa makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Valencia, mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney imefahamika atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma mawili au matatu yajayo.
Taarifa zilizotolewa na meneja wa klabu ya Man utd Sir Alex Ferguson alipozungumza na waandishi wa habari hapo jana zimeeleza kuwa mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa kipindi cha wiki mbili au tatu kufuatia majibu ya vipimo alivyofanyiwa mara baada ya kuumia kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Bolton Wanderers.
Sir Alex Ferguson amesema licha ya kutegemea mshambuliji huyo kuwa nje kwa kipindi cha majuma matatu, bado inawezekana kurejea uwanjani baada ya majuma mawili na hii inategemea na huduma ya matibabu anayoendelea kupatiwa kwa sasa huko jijini Manchester.
Kocha huyo amemzungumzi pia amemzungumzia kiungo wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Paul Scholes ambae nae anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu ambayo huenda yakamuweka nje kwa kipindi cha siku kumi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment