Mramba aangushwa na Selesaini katika jimbo la Rombo

Written By Admin on Tuesday, November 2, 2010 | 9:22 PM

Matokeo ya hivi punde yanaonyesha Basil Mramba(CCM) mmoja wa watendaji waliowahi kudumu kwa muda mrefu katika nafasi ya uwaziri ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Joseph Selasini (CHADEMA) amemwangusha Mramba baada ya kupata kura elfu 29,569 ambapo Mramba amepata kura elfu 27,649

Kwa upande wake Edwad Lowassa(CCM) ambaye pia alishika nyadhifa za uwaziri na kuwa waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu wadhifa huo mwaka 2008 ametetea jimbo lake la Monduli kwa kupata kura elfu 30,236 na kumwacha kwa mbali mpinzani wake Silanga Amani Mollel(CHADEMA) aliyepata kura 2356.

CCM pia kimeendelea kutetea majimbo yake ya Same Magharibi na Same Mashariki. Anna Kilango(CCM) amepata kura elfu 16,212 na kumwacha mpinzani wake wa karibu Neghenjwa Kaboyoka (CHADEMA) aliyepata kura elfu 6, 984 katika ambapo Dr. Mathayo David (CCM) ametetea jimbo la Same Magharibi kwa kupata kura elfu 22,906 dhidi ya mpinzani wake Eli Ikube Mduma(CHADEMA) aliyepata kura 3,989.

Huko Pangani, Salim Pamba(CCM) amepata kura elfu 9, 342 akifuatiwa na Omar Ali(CUF) mwenye kura elfu 4,521. kwa upande wa Korogwe Vijijini Ngonyani Steven(CCM) ameibuka mshindi kwa kujizolea kura elfu 41,377 ambapo mpinzani wake Siu Mohamed Maalim(CHADEMA) amepata kura elfu 3233

Jimbo la Mbozi Magharibi limechukuliwa na David Silinde(CHADEMA) ambaye amepata kura elfu 20,835 dhidi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dr. Luca Siame(CCM) aliyepata kura elfu 20,203,

Upande wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi(CCM) ametetea nafasi yake kwa kujizorea kura elfu 49,095 na kumwacha kwa mbali mpinzano wake wa karibu Allamis Mwampamba(CHADEMA) aliyepata kura elfu 31997.

0 comments:

Post a Comment