WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Serikali ya Baba Riz haitakurupuka kuitambua serikali ya mpito ya waasi wa Libya wakati bado vita inaendelea.
Kwa mujibu wa Membe, nchi za Afrika ziizoitambua serikali ya waasi wa
Libya ni pamoja na Kenya, Botswana, Ethiopia, Djibut, Rwanda na
Tunisia. Nyingine ni Senegal, Gabon, Gambia, Bokina Faso, Benin na
Nigeria. Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi 41 za Afrika ambazo bado
hazijaitambua serikali ya mpito ya waasi wa Libya.
Membe alisema Serikali ya Baba Riz inajua kwamba hatima ya Kanali
Muammar Gaddafi kuongoza Libya imekwishafikia, lakini haiwezi kuwatambua
waasi wakati bado hawajaunda serikali. “Serikali ni pamoja na kuwa na
viongozi walioapishwa, tutawatambua kama watakuwa na mihimili mitatu
ya serikali, bunge na mahakama,” alisema Membe.

0 comments:
Post a Comment